June 26, 2014

  • Hapatoshi leo Redd’s Miss Pani 2014

     
    NA  HAPPINESS MNALE
     
    KWA mara ya kwanza  kwenye ukumbi wa Maisha Plus (Pilice Mess) kutafanyika tukio la aina yake la kumsaka Redds Miss Pwani 2014 usiku wa leo.
     
    Katika Shindano hilo ambalo  litakuwa ndiyo sehemu ya kuuzinduz ukumbi huo ambao leo  hii ndiko  kutakuwa na burudani kubwa ya muziki wa dansi kutoka katika  bendi ya Extra Bongo 'Wazee wa Next level' wakiongozwa na  mzawa wa mkoa wa Pwani  Ally Choki almaarufu kama 'Mwarabu wa Kibaha' ambao nao wameahidi kutoa burudani ya kihistoria kwenye onyesho hilo.
     
    Bendi hiyo ambayo inatamba na vibao vingi ambvavyo vimeipa sika kama 'Regina' na nyinginezo (Zitaje)
     
    Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said 'Sharapova' , Otilia na wengineo watanogesha na kuacha historia siku hiyo .
     
    Katika shindano hilo jumla ya warembo Kumi watapanda jukwaani ambao  Khadija Sihaba, Glory  Jige,  Irene Rajab, Mary Samwel, Arafa Shabani, Jeniffer David, Judea Joseph, Mary Mpelo,Roksana Msangi  na Faith.
     
    Mshindi wa  Miss  Pwani ndiye atapata nafasi ya kuuwakilisha Mkoa huo  katika  shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd's Miss Tanzania 2014.
     
    Akizungumza na mwandishi wa makala hii Mkurugenzi wa Kampuni ya Linda Media Solution   (LIMSO) ambaye pia ni mratibu wa  shindano hilo  Khadija Kalili  alisema kwamba kila kitu kiko tayari hivyo ni wakati wa wakazi wa mkoa wa pwani n kujitokeza kwa wingi usiku wa leo (Ijumaa) kuja kumshuhudia mwakilishi wa   mkoa wao yaani Redds Miss Pwani 2014.
     
    Kalili aliongeza kwa kusema kuwa  anawaahidi wakazi wa mkoa wa Pwani na wilaya zake zote kwa jumla kupata burudani ya aina yake siku hiyo hiyo ni kutokana kwamba Kampuni ya Linda kuanza vema   kwa kuandaa mashindano yenye mvuto  huku akitolea mfano wa ilivyokuwa katika shindano la Wilaya ya Kibaha  mjini Redd's Miss Kibaha 2013.
     
    Kalili anasema  anatoa shukrani zake za dhati kwa wadhamini wa shindano ambao ni wadhamini wakuu  Redd's Premium Cold, DIRA Media Group,  Times FM, Radio5, Cloudes FM,  Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) ,  Montage.Kiingilio ni sh. 10,000.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.