June 27, 2014

  • MWANAMKE ALIYEASI DINI YAKE AACHIWA HURU TENA



    MWANAMKE ALIYEASI DINI YAKE AACHIWA HURU TENA
    Mwanamke wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislam ameachiliwa huru baada ya kushikiliwa kwa mara ya pili.
    Meriam Ibrahimu alikwenda katika ubalozi wa Marekani uliyopo mji Mkuu wa Khartoum.Mumewe ana asili ya Sudan Kusini lakini kwa sasa ni raia wa Marekani.Mwanamke huyo aliachiliwa baada ya kuhukumiwa adhabu ya kifo siku ya jumatatu lakini alishikiliwa tena na polisi kwa tuhuma za kughudhi hati za kusafiria ili aondoke nchini Sudan kwenda Marekani.

    Kufuatia kuachiliwa huru kwa mara nyingine, Mke huyo wa Ibrahim ameiambia BBC kwamba ataendelea kuwa Mkristo.

    Kesi yake ya kuasi dini imevuta hisia za watu wengi wakiwemo watetezi wa haki za binadamu pamoja na nchi za Magharibi.
    BBC


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.