SHIRIKA LA UMEME ZANZIBAR (ZECO)
Namba yetu
Maulizo: 024 223 8321
Dharura: 024 223 0232
Afisi Kuu
S.L.P 235,
Zanzibar – Tanzania
Simu: +255 774 334 455
Barua Pepe: zeco@zeco.co.tz
--
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limesikitishwa sana na kuzorota kwa shughuli za maendeleo kutokana na kukatika kwa umeme visiwani Unguja na Pemba kuanzia majira ya saa moja usiku hadi saa tatu usiku.
Sababu iliyopelekea kukatika huko ni kutokana na kuondoka kwa gridi ya taifa ambayo Zanzibar inapata umeme kupitia gridi hiyo.
Maeneo yote ya Unguja na Pemba yalikosa umeme na baadhi ya mikoa mingi ya Tanzania Bara iliyounganishwa na Gridi ya taifa nayo ilikosa umeme ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma na Mengineyo.
Wakati akizungumza na kituo kimoja cha habari nchini Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesim Mramba amesema ya kuwa kuzimika kwa mitambo ya kuzalisha umeme ghafla ndiko kulikopelekea kukosekana kwa umeme nchi nzima ambako husababishwa na kuzimika kwa moja ya mitambo ya kuzalisha umeme.
Katika taarifa yake amefafanua ya kuwa chanzo hasa kilichopelekea kuzimika kwa mitambo hiyo bado hakijajulikana na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa kutambua kilichosababisha katizo hilo.
Kwa upande wa Shirika la umeme Zanzibarlinasikitishwa na kukatika kwa umeme huko kwani shughuli nyingi za kimaendeleo ziliweza kusimama ikiwemo wananchi kukosa kutazama na kusikiliza maelezo ya moja kwa moja kutoka Baraza la Wawakilishi, kukosa kuangalia michezo ya kombe la dunia na kusimama kwa shughuli nyengine za kimaendeleo.
Shirika litaendelea kutoa taarifa za kina kwa vyanzo vyovyote vile vya kukatika kwa umeme na kuwaomba wananchi kuwa wastahamilivu wakati wa matukio kamahayo yanapotokea kwani husababishwa na mambo ambayo yako nje ya uwezo wa Shirika.
Shirika linapenda kutoa kuwakumbusha wananchi kuacha vitendo vya kuhujumu miundo mbinu kwa kuchimba mchanga chini ya njia za umeme kwani kuanguka kwa nguzo ya umeme ni chanzo kikubwa kinachopelekea kulikosesha taifa huduma hii muhimu ya umeme.
Imetolewa na Shirika la Umeme
Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment