June 29, 2014

  • James Rodriguez aipeleka Colombia robo fainali kwa goli la mwaka



    James Rodriguez aipeleka Colombia robo fainali kwa goli la mwaka
    Colombia imepeleka mashabiki wake wanaovutia kwa ushangiliaji wao hadi kwenye robo fainali za kombe la Dunia baada ya nyota wake James Rodriguez akifunga mabao yote. Colombia waliifunga Uruguay ya mng'ata meno Suarez bao 2-0 katika mchezo wao wa raundi ya 16 kweny uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro jana.
    Angalia goli la mwaka la Rodriguez ambalo ni tamu sana kiasi hata huchoki kuangalia. Huku goli la adui likiwa nyuma yake, kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 kwanza aliweka gambani  pasi aliyoletewa, halafu kabla mpira haujatua ardhini aligeuka na kupiga bao dakika ya 28, akiwa nje ya 18.

    Hebu cheki mwenyewe. Mambo kama haya ni marehemu Edward Chumilla tu aliyeweza kuyafanya hapa nyumbani.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.