August 20, 2014

  • Tanzania yapokea mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za Haki za Binadamu



    Tanzania yapokea mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za Haki za Binadamu
    Na Rose Masaka,Maelezo 

     Tanzania imepokea mwongozo mpya juu ya Sheria na Kanuni zinazohusu haki za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kesi kusikilizwa ili kuwapa uelewa wa kutosha wananchi juu ya haki zao za msingi.

    Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Katibu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi.Mary Massay amesema mtuhumiwa anatakiwa kumhoji polisi kosa gani amekamatwa nalo kabla ya kufikishwa kituoni.

    Bi Massay alisema wananchi wengi wamekuwa hawafahamu haki zao za msingi pindi wanapokamatwa na polisi hivyo kupelekea kuishia magerezani kwa kukosa uelewa wa haki zao za msingi. Alisema mwongozo huo umepitishwa na Tume za Haki za Binadamu Tanzania, Zimbabwe, Malawi, Tunisia na Ivory Coast na unahusu utendaji wa polisi ambapo unawataka wananchi wa Tanzania kutambua haki zao za msingi pindi wanapokamatwa na polisi.

    Akifungua mkutano huo mwandishi maalumu wa wafungwa na mazingira Kamishna Med Kaggwa kutoka taasisi ya Haki za Binadamu Uganda aliongeza kuwa Afrika inahitaji ushauri ili iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi kwa sababu kuna maeneo mengi ya kisheria ambayo yanatakiwa kufanyiwa marekebisho.

    Kamishna Kaggwa alisema mtuhumiwa kufungwa kabla ya uchunguzi kukamilika ni ukiukwaji wa sheria hivyo polisi wanatakiwa kufuata na kuheshimu sheria na kanuni zilizotungwa na nchi. Alisema kutokana na utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa asilimia 41.3 ya wafungwa wa Afrika hukuo afrika kusini ikiwa na wafungwa wengi zaidi,na asilimia 50 ya wafungwa wa Tanzania ni wafungwa wa muda mchache kati ya miaka 3 hadi 4 kupata hukumu.
    Mwandishi Maalumu wa Wafungwa Bw. Med Kaggwa kutoka Taasisi ya Haki za Binadamu ya Uganda aliyesimama akifungua Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
    Bi. Louise Edward kutoka Taasisi ya "African Policing Civilian Oversight Forum (APCOF) akitoa mada katika Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.
    Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja katika Warsha ya siku mbili juu ya mwongozo mpya wa Sheria na Kanuni za polisi kumweka mtuhumiwa chini ya ulinzi na kabla ya kusikilizwa.warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Benjamin Sawe wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHVUM


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.