June 30, 2014

  • Goli la penati dhidi ya Mexico yaipeleka Uholanzi robo fainali kombe la dunia Brazil



    goli la penati dhidi ya mexico yaipeleka uholanzi robo fainali kombe la dunia brazil leo
    Kocha wa Uholanzi Louis van Gallakimpongeza Arjen Robben kwa kufanyiwa rafu iliyozaa penati na hatimaye bao la ushindi dhidi ya Mexico leo

    Na Sultani Kipingo
    wa Globu ya Jamii
    Yaani huko Old Trafford katika  klabu ya Manchester United nchini Uingereza atakoenda kufundisha msimu ujao tayari waliishaanza kuandaa ofisi ya meneja wao mpya Louis van Gall anayeifundisha timu ya Uholanzi katika kombe la dunia, baada ya kuhisiwa kuwa ataaga mashindani hayo Jumapili hii walipocheza na Mexico. 
    Unaambiwa hadi zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo uishe, Uholanzi walikuwa bado wako nyuma kwa bao 1-0, huku kila mtu akiamini kuwa bao la kipimndi cha pili  la Mexico lillofungwa na Giovanni Dos Santos limewamaliza. 
    Lakini baada ya kazi za ziada za kipa wa Mexico Guillermo Ochoa kuzuia Uholanzo wasilete madhara, Uholanzi ambao michuano iliyopita mwaka 2010 huko Afrika ya Kusini walifia fainali, wakapiga mabao mawili ya haraka haraka na kuwaacha Mexico hoi. 
    Kwanza ilikuwa ni  Wesley Sneijder  aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 kufuatia mpira wa kona uliomdondondokea akiwa katika mkao wa kula.
    Ndipo katika dakika ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji, Arjen Robben aliangika chini baada ya kuchezewa rafu ndani ya 18. 
    Wakati huo, tayari Robben alishakataliwa penati ya wazimkatika kipindi cha kwanza kilichotawaliwa na Mexico, na bila shaka safari hii alihisi anadaiwa kitu. Kwa vyovyote vile, Klaas Jan Huntelaar aliyeingia badala ya Robin van Persie ambaye ngoma leo ilimkataa, alifunga kwa mkwaju wa chini kuipa Uholanzi tiketi ya robo fainali.
     Dakika ya sita za muda wa nyongeza katika muda wa mapumziko mafupi ya kunywa maji Arjen Robben anafanyiwa madhambi
    Wesley Sneijder  aliyesawazisha mnamo dakika ya 87 akifurahia


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.