June 25, 2014

  • NDEGE YA PAKISTAN (PIA) YASHAMBULIWA KWA RISASI




    NDEGE YA PAKISTAN (PIA) YASHAMBULIWA KWA RISASI
    Watu waliokuwa na silaha wasiojulikana jana usiku waliifyatulia risasi ndege moja ya Shirika la Ndege la Pakistan (PIA) wakati ilipokuwa ikitua katika mji ulioathiriwa na machafuko wa Pishawar nchini humo. Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 180 ilikuwa ikitokea Saudi Arabia ambapo ilishambuliwa na watu wenye silaha wakati ikijiandaa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bach Khan katika mji wa Peshawar.

    Polisi imesema kuwa risasi sita zimeipiga ndege hiyo na hivyo kupelekea kuuawa mwanamke mmoja wa Kipakistan na kujeruhiwa wahudumu wawili wa ndege hiyo.
    Hadi kufikia sasa hakuna kundi wala mtu yoyote aliyetangaza kuhusika na shambulio hilo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.