June 27, 2014

  • Shisha zimepigwa marufuku Kenya


    Shisha zimepigwa marufuku Kenya
    SHISHA 12
    Imekua ni kawaida sasa hivi kwenda kwenye sehemu mbalimbali za starehe na kukutana na huduma ya uvutaji wa Shisha (sheesha) ambayo hutolewa kwa malipo.

    Pamoja na kwamba wengi wameamini haina madhara, huko Kenya madhara yameonekana baada ya aina 19 za ladha za Shisha kugundulika kuwa zimechanganywa na dawa za kulevya ikiwemo Cocaine, Heroine, bangi na kuberi.
    Baada ya utafiti shirika la kupambana na mihadarati na dawa za kulevya nchini Kenya ndio limepiga marufuku utumiaji wa aina hizi za shisha ambapo yeyote atakaepatikana akiuza au kutumia aina hizo atafikishwa Mahakamani.

    Kwa taarifa zaidi unaweza kubonyeza play kusikiliza sauti ya Citizen TV Kenya ambayo iko mwishoni chini kwenye hii post.
    SH 1
    Baadhi ya Shisha zilizopigwa marufuku.
    SH 2



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.