June 26, 2014

  • MTUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI AOKOLEWA NA ASKARI POLISI MOSHI ,NUSURA WAENDESHA BODABODA WAMTOE ROHO

     
     
     
     
    Askari polisi wa kituo cha kikuu cha Polisi cha kati akiwa amemshikilia kijana mmoja baada ya kumokoa toka mikononi mwa madereva bodaboda ambao walikwishaanza kujichukulia hatua mkononi kwa kumuadhibu baada ya kutaka kuiba pikipiki.
    Askari katika ofisi za kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro walilazimika kufunga geti kuzuia kundi kubwa la madereva boda boda na watu wengine wakilazimisha kuingia ili kumfuata mwizi wao wa pikipiki.
    Madereva hao walionekana kukerekwa na kuzuiwa kumuadhibu kijana huyo na hapa walionekana wakilalamka.
    Jamaa wa nje akatamani kupita katikati ya Nondo hapa.
    Geti likafungwa na hakuna mtu aliyepita.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.