May 22, 2014

  • TAIFA STARS YAWASILI MBEYA KULA KIPUPWE CHA TUKUYU KUWAWINDA ZIMBABWE

     
     
     
     
    Na Baraka Mpenja
    TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars imewasili Mjini Tukuyu jijini Mbeya tayari kwa kuweka kambi ya kujiwinda na mchezo wa marudiano dhidi ya Zimbabwe mjini Harare kuwania kupangwa katua ya makundi ili kusaka tiketi ya kushiriki fainali za kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
    Stars imeamua kuweka kambi Mbeya kutokana na hali ya hali ya baridi iliyopo mkoni huko kwani inafanana na hali ya hewa ya Zimbabwe.
    Katika mechi ya kwanza iliyopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam juni 18 mwaka huu, Taifa stars iliibuka na ushindi wa mbao 1-0.
    Bao hilo pekee lilifungwa na mshambuliaji wa kati wa Stars, John Raphael Bocco `Adebayor`.
    Stars inahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kusonga hatua inayofuata.
    Kocha mkuu wa Stars, Mart Nooij baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songweni jijini humo, alisema anaamini Tukuyu ni eneo tulivu sana, hivyo vijana wake watajiandaa vizuri.
    Nooij alisema ana matumaini makubwa ya kusonga mbele katika mchezo wa marudiano ingawa anakiri wazi kuwa mechi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa.
    Mholanzi huyo aliongeza kuwa anaenda kuyafanyia marekebisho makosa ya safu ya ushambuliaji  na nafasi ya kiungo ambayo ilionekana kupwaya sana.
    Mchezo uliopita, sehemu ya beki ya kulia iliyoongozwa na Shomary Kapombe na kushoto, Oscar Joshua ilionekana kuwa na matatizo, ingawa kipindi cha pili wachezaji hawa walibadilika.
    Mwinyi Kazimoto na Frank Domayo walishindwa kuwa na uelewano katika safu ya kiungo na kuwaruhusu Wazimbabwe kucheza sana mpira.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.