June 28, 2014

  • Mbowe na Dr Slaa sasa kwisha; kushtakiwa rasmi na wajumbe Baraza Kuu!




    Mbowe na Dr Slaa sasa kwisha; kushtakiwa rasmi na wajumbe Baraza Kuu!
    Mhe Mbowe, ambae ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, na katibu mkuu wa chama hicho, Dr Slaa, wamekumbwa na pigo kubwa baada ya wajumbe wa baraza kuu kuwakalia kooni vigogo hao wawili wa CHADEMA.

    Itakumbukwa hivi karibuni wajumbe wa baraza kuu CHADEMA walitoa "press release" ya kuwatuhumu viongozi wa chama chao kwa tuhuma nzito nzito ikiwemo kukihujumu chama, ufisadi na ubadhirifu wa mali za chama. Ambapo kwa mujibu wa wajumbe hao, uhuni huu wote unafanywa na Mbowe pamoja na Dr Slaa!!!

    Lakini vilevile wajumbe wa baraza kuu CHADEMA hawajaishia kutoa tu "press release", bali wameenda mbali zaidi mpaka kwa msajili wa vyama vya siasa nchini na kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu (CAG) kwa hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi ya vigogo hao wa CHADEMA, kwa kuwa wajumbe wa baraza kuu wamejipanga kwa vielelezo vyote vya kuthibitisha ukiukwaji wa sheria katika matumizi ya mali za umma unao fanywa na Mbowe pamoja na Dr Slaa.

    Aidha, jitihada za kumtafuta Dr Slaa ili atolee maelezo suala la wao (yeye Dr Slaa na Mbowe) kushtakiwa kwa msajili wa vyama azikuweza kuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.