June 24, 2014

  • MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII,TASAF NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.



    MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII,TASAF NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.
    Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika .

    Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao utasaidia kuwaongezea kipato.

    Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku 15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari (kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
    Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.
     Pichani walengwa wa PWP katika shehia ya Mpapa wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) juu ya namna ya uibuaji wa miradi kwenye eneo lao.
    Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .




  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.