June 25, 2014

  • SUMATRA YAPATA MKURUGENZI MKUU MPYA



    SUMATRA YAPATA MKURUGENZI MKUU MPYA

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    WIZARA YA UCHUKUZI




     

     TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



    Kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali No. 30 ya mwaka 1997, Kifungu Na. 9 ikisomwa pamoja na Marekebisho yake ya Mwaka 2009, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe(MB) amemteua Bw. Gilliad Wilson  Ngewe  kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuanzia tarehe1/6/2014.

    Kabla ya Uteuzi huo Bw. G. W. Ngewe , alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA kuanzia tarehe 12/3/2014 ambapo awali alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Udhibiti wa Usafiri wa barabara, SUMATRA.
    Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 9 ya mwaka 2009 ili kusimamia usafiri wa Nchi kavu na Majini Tanzania.
    Imetolewa na:
    Katibu Mkuu
    Wizara ya Uchukuzi.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.