June 28, 2014

  • TANTRADE YATANGAZA VIINGILIO SABASABA



    TANTRADE YATANGAZA VIINGILIO SABASABA
    Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa na usalama katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kulia ni Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom.
    Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna Bulando.

    Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayo anza tarehe 28 ya mwezi juni hadi tarehe 8 mwezi julai.

    Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.

    "Viingilio vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000." Alisema Bulondo.

    "Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine."

    Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu, Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka maeneo yote ya maonesho.

    Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.

    "M pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom." Alisema Twissa.
    Malipo ya ada binafsi.

    1.      Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
    2.      Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
    3.      Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
    4.      kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
    5.      malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho   - 20,000/-
    6.      Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/- 

    Tiketi za uegeshaji magari.

    1.      Kwa siku (magari madogo)  - 4,000/-
    2.      kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
    3.      Malipo kwa pamoja – 200,000/-
    4.      Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
    5.      Maroli na magari makubwa – 500,000/-
    6.      Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-

    Maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kununua vitu mbalimbali kwa gharama nafuu na kupata fursa ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.