MANCHESTER United imekubali kumsaini kiungo wa Bayern Munich, Toni Kroos na sasa inaelekeza nguvu zake kupata saini ya mchezaji mwenzake Arjen Robben.
Dili la pauni milioni 20 kumnasa Kroos lilishaafikiwa hata kabla ya David Moyes hajatimuliwa Old Trafford, lakini kocha mpya Louis van Gaal ameunga mkono na kubariki usajili huo.
Kroos alichomoza Bayern Munich chini ya Van Gaal na sasa anataka kumtumikia tena kocha wake wa zamani.
Robben mwenye umri wa miaka 30 hivi karibuni alisaini mkataba mpya wa miaka mitatu, lakini inaaminika hatapenda kumwangusha kocha wake wa timu ya taifa ambaye atakuwa naye katika michuano ya Kombe la dunia.
Mshambuliaji huyo alikuwa mtu wa kwanza kusajiliwa na Van Gaal Bayern Munich kwa pauni milioni 20 mwaka 2009 kutoka Real Madrid.
Inaaminika pia kuwa United imeshamalizana beki wa kushoto wa Southampton Luke Shaw kwa pauni milioni 27 huku beki wa kati wa Borussia Dortmund, Mats Hummels akiwa kwenye rada za Van Gaal.
0 comments:
Post a Comment