Serikali
imeshauriwa kuweka mgawanyo sawa ya utekelezaji katika miraji ya Maji
nchini ili kuondoa tatizo sugu la Maji kwa maeneo yenye ukame na
upungufu mkubwa wa Maji.
Akichangia
wakati wa bajeti ya Wizara ya Maji, mbunge wa Singida Mashariki Mh
Tundu Lissu alisema imefika wakati serikali lazima iweke uwiano sawa wa
mgawanyo wa fedha za miradi ya maji kwenye mikoa na sehemu zenye
upungufu mkubwa wa Maji hapa nchini.
Akitolea
mfano jimboni kwake alisema bajeti ya mwaka huu kwa jimbo lake la
Singida Mashariki jumla ya Milioni 839 zimetengwa kwa ajili ya jimbo
lake. Alipongeza serikali kwa miradi miwili ya Maji iliyoanza
kutekelezwa jimboni kwake katika wilaya ya Ikungi na Mungwaa na kwamba
ukarabati wa visima vilivyojengwa na taasisi ya Catholic Service Relief
(CSR) ukiendelea.
Aliongeza
kuwa kwa mikoa yenye vyanzo vya Maji kama vile Mito na Maziwa ni muhimu
fedha kidogo zikatumika na nguvu nyingi ikaelekezwa kwenye maeneo yenye
ukame mkubwa wa Maji kama vile Singida, Dodoma, Shinyanga na Simiyu.
Mbunge
wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu akichangia hoja ya wizara ya Maji
wakati wa Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka
2014/2015.
0 comments:
Post a Comment