Afisa wa Jamii Mji Mdogo wa Makongolosi, Nkongoki Ezekiel kwa niaba ya Mbeya yetu blog akimkabidhi mtoto Elizabeth Tanzania mafuta chupa moja ya kujikinga na jua
WATOTO wenye ulemavu wa ngozi(ALBINO) wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wanaomba msaada wa kupatiwa mafuta ya kuzuia mwanga wa jua unaoathiri ngozi zao. Maombi hayo yalitolewa na zaidi ya watoto sita wenye ulemavu wa ngozi wanaoishi Makongolosi Wilaya ya Chunya mkoani hapa ambao wanakabiliwa na ukosefu wa mafuta ya ngozi,miwani ya kusomea na kofia ili kuweza kukabiliana miale ya jua. Mama Mzazi wa watoto hao, Sophia Edward(30) alisema wanawe Lusekelo Tanzania(13) anayesoma darasa la saba na Elizabeth Tanzania(8)anayesoma darasa la tatu wanakabiliwa na ukosefu mafuta,kofia na miwani ya macho kwa muda mrefu hivyo kuwafanya watoto hao kuwa na wakati mgumu kutokana na joto kali hali iliyopelekea ngozi zao kuharibika. Kwa upande wake Afisa wa Jamii Mji Mdogo wa Makongolosi, Nkongoki Ezekiel alisema kuwa watoto hao kwa mara ya mwisho walipata mafuta miezi sita iliyopita. Alisema mafuta hayo ni adimu na wao hawana namna yoyote ya kufanya hivyo kuwaomba wasamaria wema wenye mafuata,miwani na kofia kuwasaidia ili wakabiliane na changamoto zinazowakabili. Aidha alisema mbali ya changamoto hiyo watoto hao wamekuwa na maendeleo duni katika masomo kutokana na udhaifu wa kuona vema hivyo kushindwa kuona vizuri na wingi wa wanafunzi katika darasa kunawafanya kuwa nafasi chini. Mama mzazi wa watoto hao alisema kipato duni kimesababisha watoto kuwa na matokeo hafifu kwani kipato chao kinatokana na Baba mzazi Bwana Tanzania Mwakatobe(46)kutegemea uchimbaji wa madini ndipo wapate riziki hivyo kushindwa kuwapeleka shule maalumu. Mwisho.
Na Mbeya yetu |
0 comments:
Post a Comment