June 03, 2014

  • SHUKRANI ZA ZITTO KABWE BAADA YA MSIBA WA MAMA YAKE



    SHUKRANI ZA ZITTO KABWE BAADA YA MSIBA WA MAMA YAKE
    Tumempumzisha mama kwenye nyumba yake ya milele, jirani na alipopumzishwa baba yake mzazi. Nawashukuru sana nyote kwa salam zenu za pole.
    Nawashukuru nyote mlioweza kufika kigoma kumsitiri mama. Sina cha kuwalipa, mola atawalipa.
    Nawashukuru sana wakazi wa Manispaa ya Kigoma, jimbo la Kigoma Kaskazini na wana Kigoma wote. 


    Nawashukuru watanzania. Madaktari wote waliomhudumia mama, wahudumu wa hospitali, maafisa wa Bunge na wabunge wenzangu. Mola awazidishie katika shughuli zenu.
    Mama yangu alikuwa nguzo kubwa kwangu na familia yetu. Mti mkubwa umeanguka. Mola amempenda zaidi mama. Pumzika kwa Amani.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.