June 16, 2014

  • Semina ya Wabunge Marafiki wa Mazingira kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Change)





    Semina ya Wabunge Marafiki wa Mazingira kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (Climate Change)
    Chama cha Wabunge Marafiki wa Mazingira (TAPAFE),kwa kushirikiana na Baraza la Usimamizi wa Mazingira,na Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP),wameandaa semina kwa ajili ya wajumbe wa chama hicho mjini Dodoma,jumamosi tarehe 14 Juni 2014 na jumapili tarehe 15 Juni 2014 kuhusu Athari za Mabadiliko ya Tabianchi katika Maendeleo ya Nchi.
    Waziri wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais,Prof. Mark Mwandosya akitoa mada Kuhusu Changamoto za Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria na Bonde la Mto Nile.
    Mheshimiwa Dr. Binilith Mahenge,Waziri wa Nchi (Mazingira) akifungua rasmi semina hiyo.Kushoto kwake ni Mhe. Cynthia Ngoye,Mwenyekiti wa TAPAFE.
    wajumbe wakisikiliza kwa makini mada inayotolewa.
    wanachama na wa TAPAFE wakiwa pamoja baada ya kuhitimisha Semina.Waliokaa kutoka kushoto ni Dr Vedast Makota,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC;Mhe.Anastazia Wambura;Mhe Lediana Mng'ong'o;Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Nchi (Kazi Maalum) Ofisi ya Rais;Mhe. Cynthia Ngoye,Mwenyekiti wa TAPAFE;Mhe. Dr Binilith Mahenge,Waziri wa Nchi (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais;Mhe Lolesia Bukwimba,Katibu wa TAPAFE;Mhe.Susan Kiwanga; na Mhe.Luckson Mwanjale.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.