June 18, 2014

  • MARIO BALOTELLI ANUKIA KUTUA ARSENAL



    MARIO BALOTELLI ANUKIA KUTUA ARSENAL

    Realistic signing: Arsenal chiefs believe Balotelli                is a realistic target with AC Milan lowering their wage                bill

    MARIO Balotelli amefungua milango ya kujiunga na Arsenal baada ya wakala wake kusema "lolote linawezekana" kiangazi hiki.

    Mshambuliaji huyo wa Italia amabaye alifunga goli la ushindi dhidi ya England Jumamosi usiku, amekuwa akihusishwa kwa kiwango cha juu katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Arsene Wenger.

    Kocha wa Arsenal amepania kusajili mshambuliaji wa uhakika ili kujipanga vizuri katika kusaka taji la Ligi Kuu msimu ujao.

    Arsenal iliwasiliana na wakala wa Balotelli, Mino Raiola ili kuangalia uwezekano wa kupeleka ofa ambapo Raiola alionyesha kuvutiwa.

    "Arsenal ni klabu bora," aliiambia Sky Sports. "Usajili huu utawezekana? Lolote linaweza kutokea," aliongeza wakala huyo wa Balotelli.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.