ARJEN Robben wa Holland, ameweka rekodi mpya ya kuwa mwanasoka aliyekimbia kwa kasi zaidi.
Winga huyo wa Bayern Munich alitoka kwenye nusu yake na kumkimbiza beki wa Hispania Sergio Ramos hadi kumpita na kwenda kufunga moja kati ya mabao matano waliyowatungua mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia.
Viwango vya FIFA vimebaini kuwa kasi hiyo ilikuwa ni sawa na kilomita 37 kwa saa ambayo haijawahi kuwekwa na mwanasoka yeyote hapo kabla.
Rekodi za nyuma ni kama ifuatavyo: Theo Walcott 35.7, Antonio Valencia 35.2, Gareth Bale 34.7, Aaron Lennon 33.8, Cristiano Ronaldo 33.6, Lionel Messi 32.5, Wayne Rooney 32.1
0 comments:
Post a Comment