KOCHA wa Al Arabi ya Qatar, Dan Petrescu amesema nyota wa Barcelona Xavi Hernández amekubali kujiunga na timu yake.
Petrescu ambaye ni beki wa zamani wa Chelsea, amesisitiza kuwa kiungo huyo wa Hispania tayari amesaini mkataba wa awali wa kukipiga Al Arabi.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Rumania, Xavi, 34 atalipwa zaidi ya pauni milioni 6 kwa msimu kama usajili wake utakamilika.
Xavi ameitumikia Barcelona kwa muda wake wote wa soka lakini sasa anaamini kuwa wakati wake wa kutafuta changamoto mpya umewadia.
0 comments:
Post a Comment