June 13, 2014

  • MAJI KERO KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MPANDA NDOGO, WASAFIRI KILOMITA MBILI KUPATA HUDUMA


    MAJI KERO KWA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MPANDA NDOGO, WASAFIRI KILOMITA MBILI KUPATA HUDUMA
    s9Wanafunzi wanahitaji kisima cha maji Mpanda
    Na Kibada wa Kibada -Katavi
    Shule ya Msingi Mpanda ndogo katika halmashauri ya wilaya ya Mpanda inakabiliwa na changamoto ya maji hali inayowalazimu wanafunzi
    kufuata maji kwenye mto uliopo kijini cha jirani  kilicho umbali wa kilomita 2.

    Hayo yameelezwa na walimu wanaofundisha katika shule hiyo walipokuwa wakizungumza na mbunge wa jimbo la mpanda Vijijini , Moshi Kakoso aliyefanya ziara shuleni hapo  hivi karibuni na kupata nafasi ya kuzungumza na walimu kupata changamoto zinazowakabili pamoja na kukagua maendeleo ya miradi inayotekelezwa.
    Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa shule hiyo, Rashidi Msyete alieleza changamoto mbalimbali zinazoikabili shule ikiwemo utoro kwa kwa baadhi ya wanafunzi,uhaba wa vitabu vya masomo ya sayansi , shule kutokuwa na mlezi hasa kwa wanafunzi wa kike (Matroni).
    Alisema kutokana na kukosa maji wanafunzi inawalazimu kuvunja masomo na kufuata maji umbali mrefu hali inayowafanya kupoteza muda mwingi nje ya vipindi vya madarasani.
    Kutokana na kuwepo kwa changamoto hiyo walimwomba mbunge kusaidia kwa njia moja au nyingine kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.
    Kwa upande wake mbunge  Kakoso aliagiza kamati ya maendeleo ya Kata kukaa na uongozi wa Halmashauri kuangalia kwenye mfuko wa jimbo ambalo upo kwa ajili ya kusaidia maendeleo katika jimbo waletewe maji ikiwa ni pamoja na kuchimbiwa kisima katika shule hiyo ili kuondoa kero hiyo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.