"Brazuca" si kitu kingine bali ni jina la mpira unaotumika katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea chini Brazil hivi sasa.
Neno hilo lina maana mbili. Ya kwanza ni neno la nchi hiyo kwa wa-Brazil wanaoishi nje ya nchi – yaani Diaspora. Maana ingine, neno hilo lina maana ya kujivunia, kuufurahia na kutambia u-Brazil kwa watu wa nchi hiyo, ama kitu ama jambo lolote la kusisimua linalohusiana na nchi hiyo.
Baadhi ya mipira ya Kombe la Dunia imekuwa maarufu kuliko mingine, huku wachezaji wakiilalamikia kwa kile wanachosema mipira hiyo husafiri kwa kasi zaidi hewani, kiasi hata kusumbua walinda milango
Adidas, watengenezaji maalumu wa mipira kwa ajili ya Kombe la Dunia tokea mwaka 1970, waliuita "Jabulani" mpira uliotumika katika fainali hizo mwaka 2010 huko Afrika Kusini, na kulakiwa na kila aina ya makelele kuwa mwendo wake hautabiriki.
Huu wa sasa jina lake rasmi ni "Adidas Brazuca" na umetengenezwa na kampuni ya Forward Sports ya Sialkot nchini Pakistan. Jina "Brazuca" la mpira huo lilizinduliwa September 2, 2012 jijini Rio de Janeiro, kupitia kura ya maoni iliyoendeshwa na Fifa na Adidas, ambapo wapiga kura zaidi ya milioni moja wa Brazil walilichagua kwa kura 77.8% dhidi ya majina mengine mawili yaliyopendelkezwa – "Bossa Nova (14.6%) na Carnavelesca (7.6%)
0 comments:
Post a Comment