Kutokana na vurugu zilizofanywa na baadhi ya wamachinga jijini Mwanza, ghasia hizo zimezua sura mpya ya kudai viongozi wa Halmashauri ya jiji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) walipokea fedha kutoka katika misikiti mitatu ili kuwaondoa wafanyabiashara wanaoziba misikiti hiyo.
Katika jiji la Mwanza leo hali imekuwa shwari isipokuwa eneo moja la Makoroboi, eneo la misikiti machinga waliovunjiwa vibanda vyao vya biashara wamekusanyika wakiendelea kutoa madai ya kuwa serikali inawaonea.
Katibu mwenezi wa wa CCM wa Mkoa Simoni Mangelepa amekanusha uvumi uliopo kuwa wafanyabiashara hao wamenyimwa haki ya kufanya biashara katika eneo lote la Makoroboi .
"Si kweli kwamba tumewanyima machinga hawa kuuza bidhaa zao katika eneo lote la Makoroboi bali ni machinga waliozingira eneo la kuabudu iliyoko misikiti mitatu, niwaombe viongozi wa wamachinga wanapoenda katika vikao na kukutana na viongozi wa Halmashauri ya jiji, viongozi wa machinga wasiwapotoshe wamachinga bali wawaelimishe wafanyabiashara wao kuwa waende katika maeneo waliyopangiwa na halmashauri," alisema Simoni.
Aidha ameeleza kuwa Halmashauri ilitenga maeneo 11 kupitia wilaya zote mbili, wilaya ya Ilemela na Nyamagana kwa ajili ya wamachinga cha ajabu waligoma kuondoka eneo la misikiti mitatu wanakoabudu Wahindi, maeneo waliondolewa ni halali Chama cha Mapinduzi kinawapenda wafanyabiashara wote na kila raia ana haki ya kuabudu kwa uhuru.
Kwa mijibu wa oparesheni inayoendelea jijini Mwanza kwa ajili ya kuweka mji safi tangu kuanza Mei 17 hadi kufikia Juni 11 lengo ikiwa ni kusafisha jiji, mfanyabiashara anapofanya biashara eneo lolote bila kufuata utaratibu anachukuliwa hatua na serikali, vile vile anakuwa anachafua mji ndio mana kuna maeneo maalumu ya biashara na kufuata utaratibu wa halmashauri.
Wamachinga wanaofuata utaratibu uliopo watafanya shuguli zao kwa amani na hawatafuatwa na kiongozi yeyote wa serikali, sisi kama serikali hatuwanyanyasi wamachinga tunatambua kuwa wamekopa mikopo mbalimbali kwa nia ya biashara na wanapaswa kurejesha hivyo ni vema wakatii sheria na si kuleta vurugu.
Nitoe rai kwa viongozi wa machinga na wafanyabiashara ndogondogo wawaelimishe wafanyabiashara wao kwa kuwaeleza waende katika maeneo waliyopangiwa ili kuwapisha waumini wa misikiti mitatu waabudu kwa uhuru kama ilivyo katika madhehebu mengine.
0 comments:
Post a Comment