June 04, 2014

  • YUOTUBE YAONDOLEWA UTURUKI


    YUOTUBE YAONDOLEWA UTURUKI
    Mahakama ya juu zaidi imesema kuwa marufuku ya Youtube ilikiuka uhuru wa watu kujieleza
    Serikali ya Uturuki imeondoa marufuku ya miezi miwili iliyowekwa dhidi ya mtandao wa kijamii wa YouTube .

    Hatua hii inakuja baada ya mahakama ya juu zaidi nchini humo kuwaamuru maafisa wakuu kurejesha huduma za mtandao huo, ikisema kuwa marufuku hiyo ilikiuka sheria za uhuru wa kujieleza.
    Marufuku hiyo iliwekwa mwezi Machi , baada ya kanda kuhusu madai ya ufisadi nchini humo kusambazwa kwenye mtandao huo.
    Moja ya kanda zilizopeperushwa ilionyesha maafisa wakuu wa jeshi wakizungumzia nyenzo za kuingilia vita vya Syria na wengine wakiongea kuhusu ufisadi wakuwahusisha maafisa wakuu wa serikali ambao ni washirika wa Erdogan
    Uturuki ilipitisha sheria yenye utata mapema mwaka huu ambayo iliwaruhusu wenye kutoa huduma hiyo kuikomesha bila kufuata amri ya mahakama.
    Serikali pia iliweka marufuku kwa mtandao wa kijamii wa Twitter,ingawa marufuku hiyo iliondolewa mwezi jana.
    Maafisa wakuu waliendelea kubana YouTube hadi Jumanne licha ya uamuzi wa mahakama ukitoa wito kwa serikali kuondoa marufuku hiyo.
    Uamuzi huo wa mahakama ya juu zaidi pia unaonekana kama kupuuza serikali ya waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan, ambayo imekuwa ikikosoa vikali mitandao ya kijamii.

    YouTube imewahi kubanwa tena nchini Uturuki mwaka 2007, lakini marufuku hiyo iliondolewa mwaka 2010.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.