June 08, 2014

  • TANGAZO LA KUNYONGWA KWA MUSLIM BROTHERHOOD


    TANGAZO LA KUNYONGWA KWA MUSLIM BROTHERHOOD
    Mahakama moja nchini Misri imewahukumu vifo viongozi kumi wa kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood kwa kuchochea ghasia zilizosababisha vifo vya watu wawili mwezi July.Washtakiwa wengine 38 akiwemo kiongozi wa kundi hilo Mohammed Badie watapewa hukumu yao ifikiapo mwezi ujao.
    Raia hao walipatikana na hatia ya kuchochea uma na kuzuia msafara wa magari katika mji wa Qalyub kazkazini mwa mji wa Cairo.
    Wamekuwa wakishiriki katika maandamano dhidi ya jeshi ambalo lilimpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi. Bwana Badie tayari amehukumiwa kunyongwa katika kesi nyengine.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.