June 09, 2014

  • TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI




    TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
    DSC00207
    MTU MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA WLLIAM KABINJI (38) MKAZI WA KIJIJI CHA MANTENGU [A] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KINACHODHANIWA KUWA NI PANGA SEHEMU ZA USONI  NA JUU YA  JICHO LA KUSHOTO KISHA KUNYONGWA SHINGO NA KUTUNDIKWA JUU YA  MTI AKIWA AMEFUNGWA SHINGONI KWA KUTUMIA  KITENGE.TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA KATIKA KIJIJI CHA ILEMBO, KATA YA VWAWA, TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA MAUAJI HAYO NI KULIPIZA KISASI BAADA YA  MAREHEMU KUCHOMA MOTO NYUMBA TATU ZA JIRANI ZAKE  NA KUITEKETEZA KABISA NYUMBA YA ELIAS MWAMLIMA (32) MKAZI WA KIJIJI CHA MANTENGU [A]  TAREHE 04.06.2014 MAJIRA YA  SAA 21:30 USIKU NA KUTOROKA.

    JITIHADA ZA KUWASAKA NA KUWAKAMATA WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AMBAO NI MAJIRANI WANAOFAHAMIKA ZINAENDELEA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
    KATIKA TUKIO LA PILI:
    MTEMBEA KWA MIGUU ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA EZEKIEL KYANDO (72) MKAZI WA BAGAMOYO AMEFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MAKANDANA – TUKUYU KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGWA NA GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA.
    TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI KATIKA ENEO LA BAGAMOYO TUKUYU MJINI, KATA YA BAGAMOYO, TARAFA YA TUKUYU KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA. UCHUNGUZI UNAONYESHA KUWA CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI HIYO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
    TAARIFA ZA MISAKO:
    JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA NONDE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SAMSON JULIUS (18) AKIWA NA BHANGI KETE 68 SAWA NA UZITO WA GRAMU 340.
    MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 08.06.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI KATIKA ENEO LA STENDI KUU YA MABASI, KATA NA TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA.
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA TABIA YA KUTUMIA BHANGI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YAKO
    Imetolewa na:
    [AHMED Z. MSANGI – SACP]
    KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.