June 07, 2014

  • Rais mpya wa Ukraine kuapishwa



    Rais mpya wa Ukraine kuapishwa
    Poroshenko alikutana kwa mara ya kwanza na Rais wa Urusi Vladimir Putin Alhamisi
    Rais mteule wa Ukraine Petro Poroshenko amepongeza mkutano wake na rais wa Urusi Vladmir Putin kama mwanzo wa majadiliano kuhusu mzozo unaondelea mashariki mwa Ukraine.

    Bwana Poroshenko ambaye anatarajiwa kuapishwa rasmi kama kiongozi wa taifa hilo hilo amesema kuwa mazungumzo mengine na Urusi yatafanyika hapo kesho siku ya Jumapili.

    Vilevile amemuonya bwana Poroshenko kwamba iwapo Ukraine itaingia katika mkataba wa kibiashara na muungano wa Ulaya,Urusi itachukua hatua za kuutetea uchumi wake.Bwana Putin amesema kuwa vita vinafaa kusitishwa katika eneo hilo kabla ya majadiliano kuanza.

    Viongozi hao wawili walikutana pembezoni mwa siku ya kusherehekea wakongwe wa vita mjini Normandy nchini Ufaransa.
    Ni mkutano wa kwanza tangu kuchaguliwa kwa bwana Poroshenko mnamo mwezi Mei.
    Kiev inatuhumu Moscow kwa kuunga mkono wapiganaji wa maeneo ya kusini mwa nchi wanaotaka kujitenga,madai ambayo Kremlin imekanusha.
    Mapigano yaliendelea Ijumaa huku waasi wanaounga mkono Urusi, wakiripotiwa kudungua ndege ya serikali karibu na eneo linalodibitiwa na waasi la Sloviansk.
    Msemaji wa jeshi la Ukraine aliambia vyombo vya habari kwamba ndege hiyo ilikuwa inabeba chakula cha msaada , lakini taarifa hizi hazijaweza kuthibitihshwa.

    Awali wanajeshi wa serikali walifanya mashambulizi karibu na mji huo.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.