June 16, 2014

  • Rais Kikwete ateta na Wasanii Dodoma




    Rais Kikwete ateta na Wasanii Dodoma
    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisistiza jambo wakati akizungumza na msanii wa kizazi kipya Ommy Dimpoz ikulu ndogo mjini Dodoma wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi.Kulia ni mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete.
    Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza kwa makini mwanamuziki wa kizazi kipya Diamond platinum wakati chakula cha usiku alichowaandalia wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendo na Uzinduzi wa Video ya wimbo maalum wa miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma jumamosi iliyopita(picha na Freddy Maro).


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.