June 16, 2014

  • Mateso Taleban lawakata vidole raia waliopiga kura kama adhabu.



    Mateso Taleban lawakata vidole raia waliopiga kura kama adhabu.
    taliban1

    Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kaskazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi ya pili.Katika tukio jengine kundi la Taleban limewakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.
    Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.

    taliban
    Raia wa taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa Waziri wa mambo ya kigeni Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuwa waziri wa fedha.
    Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.