June 18, 2014

  • Kipa wa Mexico ainyima Brazil ushindi


    Kipa wa Mexico ainyima Brazil ushindi
    Kipa Francisco Ochoa aliokoa mikwaju tele ya Brazil
    Na BBC 
    Mexico walipata pointi moja dhidi ya Brazili, katika mechi ya kundi A iliyomalizika bila ya timu yeyote kutisa wavu wa mwenziye katika uwanja wa Estadio Castelao huko Fortaleza Usiku wa kuamkia leo.
    Brazil walishindwa kufunga bao na ilikua sio kama timu ile iliyoishinda Croatia mabao 3-1 matika mechi ya ufunguzi .
    Brazili walimiliki asilimia kubwa ya mchezo hata ingawa hawakuitumia kwa manufaa yao.Hata hivyo Brazil inamlaumu Kipa wa Mexico Francisco Ochoa, aliyefanya kazi ya ziada katika mechi hiyo kuhakikisha vijana wa Luiz Felipe Scolari hawajizolei alama zote tatu.
    Licha ya Mashambulizi ya Neymar ,kipa wa mexico Ochoa alihakikisha mechi hiyo inaisha sare tasa.
    Mshambulizi wa Mexico, Oribe Peralta alijaribu ngome ya Brazili lakini Thiago Silva na Marcelo walimzuia.
    Ochoa tena aliokoa jaribio lingine la Neymar katika kinyang'anyiro katika lango la Mexico.
    Jaribio lingine la Jo lilizuiwa na Ochoa; kipa wa Mexico.
    Kisha mpira wake Silva, kwa kichwa, kutoka kwa kona yake Neymar, ukasimamishwa tena na Ochoa katika dakika ya 85.
    Wito wa Brazili wapewe penalti Marcelo alipoanguka kwa urahisi mbele ya lango la Mexico uliambulia patupu.Mexico kwa upande wao hawakuwa na nafasi nyingi, ila wakati ule Hector Herrera alipiga mkwaju uliopita kidogo juu ya lango la Brazil.


    Matokeo haya yanaziwacha timu zote mbili zikiwa na alama nne katika kundi lao, zikiwa zimesalia na mchezo mmoja kucheza.




  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.