June 11, 2014

  • Serie A News: Andrea Pirlo asaini miaka miwili Juventus


    Serie A News: Andrea Pirlo asaini miaka miwili Juventus
    Kiungo wa kimataifa wa Italia Andrea Pirlo amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuichezea Juventus ambapo atabaki klabuni hapo hadi 2016.
    Pirlo, 35 amekuwa na Juventus tangu mwaka 2011 baada ya kuiwacha AC Milan na ameichezea klabu hiyo michezo 131 akiisaidia kutwaa taji la Serie A mara tatu mfululizo.
    Msimu uliopita, Pirlo alicheza michezo 43 na kufunga magoli sita ambapo Juventus ilishinda ligi kwa kuweka rekodi ya kuwa na pointi 102.
    Kwa sasa Pirlo yuko nchini Brazil akiwa na timu ya taifa ya Italia kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia ambayo yanaanza kesho Alhamisi.
    Italia itafungua michezo yake ya Kundi D dhidi ya England siku ya Jumamosi, kabla ya kuumana na Costa Rica Juni 20 na Uruguay siku nne baadaye.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.