REDIO tatu zenye majina na masafa marefu zimejitosa kutangaza shindano la Redd's Miss Pwani 2014.
Akizungumza jana Mratibu wa shindano hilo Khadija Kalili alisema kwamba amepata udhamini wa matangazo kutoka Redio 5, Times FM na Redio Clouds FM.
Kalili alisema kwamba hivi sasa joto kwa warembo limepanda huku kila mmoja akiwa na ari ya kunyakua taji hilo siku hiyo Juni 27.
Redd's Miss Pwani imepangwa kufanyika Juni 27 mwaka huu kwenye ukumbi wa Maisha Plus (Police Mess).
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa bendi ya muziki wa dansi ya Extra Bongo inayoongozwa na mwanamuziki mkongwe nchini Camarade Ally Choki ndiyo itakayopamba shindano hilo.
Mbali ya Choki ambaye atakuwa na kikosi chake kikali cha wacheza shoo kinachoongozwa na Mussa Hassan Nyamwela pamoja na wanenguaji wa kike kama Maria Soloma , Asha Said 'Sharapova' , Otilia na wakali wengine.
Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Linda Media Solutions (LIMSO).
Alisema katika shindano hilo warembo 12 watapanda jukwaani ikiwa ni katika kumsaka malkia wa Mkoa wa Pwani ambaye atakuwa mwakilishi katika shindano la kanda ya Mashariki na baadaye katika fainali za Redd's Miss Tanzania 2014 zitakazofanyika baadaye mwaka huu.
Kalili aliwataja wadhamini wa Miss Pwani ni Redd's Premium Cold, DIRA Media Group, Eden Herbalist Clinic ya Jijini Dar es Salaam, CXC Africa, Kitwe Traders, Michuzi Media Group, Jambo Concept Tanzania Limited, Bongoweekend.blogspot.com, Maisha Plus (Police Mess) , Montage, Filbert Bayi Foundation (FBF).
Kiingilio ni sh. 10,000.
Hao pichani ni baadhi ya washiriki.
0 comments:
Post a Comment