June 23, 2014

  • NDG. Nehemia Mchechu ndiye mwenyekiti mpya wa Bodi ya SBL



    NDG. Nehemia Mchechu ndiye mwenyekiti mpya wa Bodi ya SBL
    Kampuni ya Serengeti Breweries Limited ( SBL ) leo inatangaza utuezi wa Ndg. Nehemia Mchechu kama Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya SBL. Uteuzi wa Ndg. Mchechu unafuata ukamilisho wa umiliki wa Mhe. Jaji (mstaafu) Mark Bomani . Katika nafasi yake mpya , Bw Mchechu pia atakukwa memba ya bodi ya kampuni ya bia ya East Africa.

    Ndugu Nehemia Mchechu kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Nyumba la Taifa( NHC) . Bw. Mchechu anauzoefu mkubwa katika masuala ya fedha na usimamizi. Hapo awali alishika nafasi muhimu katika sekta ya benki , hasa kama Mkuu wa Masoko Kimataifa na mkurugenzi msaidizi benki ya Standard Chartered, na kuwa Mkurugenzi Mtendaji benki ya Commercial Bank of Africa Tanzania (CBA) .

    Ndugu Mchechu ana Shahada ya Biashara (Fedha) na Utawala ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Yeye pia ni Rais wa Umoja wa wanfunzi waliomaliza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Biashara na mwanachama wa ACI – Financial Market Association Tanzania.

    Miongoni mwa nafasi nyingine muhimu, Ndugu Mchechu pia ni Mkurugenzi na mwanachama wa CEORT na pia ni Mkurugenzii wa TIC.

    SBL inachukua fursa hii kumkaribisha na kumpongeza Mwenyekiti wake mpya wa bodi na kuwashukuru mwenyekiti wa bodi Mheshimiwa Bomani kwa mchango wake bora na wa kipekee wakati wa uongozi wake.
    Mwenyekiti wa Bodi ya SBL aliemaliza muda wake,Mh. Mark Bomani akimpongeza mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo,Ndg. Nehemia Mchechu mara baada ya hafla ya kumpongeza.
    Picha ya pamoja na Sehemu ya Wakurugeni wa SBL.
    Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya SBL,Ndg. Nehemia Mchechu akizungumza machache kwenye hafla hiyo.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.