June 23, 2014

  • Vodacom yaleta gulio jingine la mauzo ya bidhaa za Mawasiliano



    Vodacom yaleta gulio jingine la mauzo ya bidhaa za Mawasiliano
    Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutangaza gulio la bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu na ipad za kisasa lililoandaliwa na kampuni yake Juni 28 na 29 katika viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es salaam. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu. Hii ni mara ya pili kwa Vodacom kuandaa gulio la aina hiyo ikiwahusisha watengeneza bidhaa za simu za mkononi.

    Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeandaa gulio kubwa la wazi kwa ajili ya mauzo ya bidhaa mbalimbali za simu, ipad na bidhaa nyengine zinazofanana na hioz kwa lengo la kuwakwezesha wateja wake na watanzania kwa ujumla kupata simu hizo kwa gharama nafuu zaidi ya gharama za kawaida za sokoni.

    Gulio hilo maarufu kwa jina la Vodacom Expo ni la pili kuandaliw ana Vodacom na linatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululizo kuanzia tarehe 28 na 29 mwezi huu katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

    Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Salum Mwalim amebainisha kuwa Vodacom Expo ni tukio kubwa ambalo wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla hupata fursa ya kununua simu za kisasa na bidhaa za mawasiliano zenye ubora kwa bei ya chini tofauti na wanazouziwa madukani.

    "Mwaka jana kwa mara ya kwanza tulipoitisha gulio hili tulishuhudia idadi kubwa ya watu wakifurika kwa ajili ya kupata bidhaa mbalimbali za simu za mkononi, hali hiyo ilitupatia ujumbe kuwa wazo tulilolibuni limepokelewa vema na watanzania na kwmaba ipo haja ya kurudio tena tukio hilo ili tuwapatie tena fursa ya kupata simu za aina mbalimbali kwa gharama nafuu zaidi."

    Mwalim amesema uamuzi wa kufanya gulio hilo katika viwanja vya Leaders ni kuweza kukabiliana na changamoto ya msongamano wa watu kufuatia idadi kubwa ya watu wlaiohudhuria gulio la mwaka jana.

    Akizungumzia baadhi zitakazopatikana siku hiyo, Mwalim amesema "Safari hii simu za kisasa zikiwemo za smartphone ni nyingi zaidi kutoka makampuni tofauti na kizuri zaidi zitakuwa zimeunganishwa na ofa za vifurushi mbali mbali kutoka Vodacom kama vile muda wa maongezi, sms na intaneti."Aliongeza

    Mwalim amesema kuw lengo la Vodacom ni kutaka kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uwezo wa kumiliki simu bora na ya kisasa kwa ajili ya mawasiliano ya sauti na huduma za intanenti ili kuendana na aksi ya maendeleo kwenye huduma za simu za mkononi ambayo Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayoendelea.

    "Kupitia mtandao wetu tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kumuwezesha kila mtanzania kumudu kumilki smartphone. Ningependa kuwaondoa shaka wateja wetu kuwa safari hii bidhaa ni nyingi, bei nafuu, muda wa manunuzi umeongezwa zaidi na hii yote ni kutokana na maoni tuliyoyapokea kutoka kwenu na kuyafanyia kazi, naomba mjitokeze kwa wingi siku hiyo."Aliongeza Mwalim.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.