June 02, 2014

  • MUME WA FROLA MBASHA AJITOKEZA...ATOA SIRI NZITO...KUWAKABILI POLISI



    MUME WA FROLA MBASHA AJITOKEZA...ATOA SIRI NZITO...KUWAKABILI POLISI
    Emmanuel Mbasha, ambaye ni mume wa mwimbaji nguli wa nyimbo za Injili, Flora Mbasha amejitokeza hadharani na kusema kwamba atakwenda polisi mwenyewe kujibu tuhuma dhidi yake za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
    Faili la tuhuma dhidi ya Mbasha lilifunguliwa Jumatatu iliyopita katika Kituo cha Polisi Tabata (Tabata Shule) wakati shemejiye huyo (jina tunalihifadhi), alipotaarifu kuwa Mbasha alimbaka mara tatu kwa siku mbili tofauti. Kesi hiyo ilipewa namba TBT/RB/3191/2014 na TBT/IR/1865/2014.
    Tangu siku hiyo, polisi imekuwa ikieleza kuwa inamsaka Mbasha bila ya mafanikio lakini mwishoni mwa wiki mtuhumiwa huyo aliongea na gazeti hili na kuelezea upande wake wa tukio hilo na kwamba yuko tayari kujisalimisha ili ukweli ubainike.
     Tuhuma dhidi yangu ni za kutengeneza
    alisema Mbasha na kufafanua kuwa yote hayo yanatokana na mgogoro wa kifamilia baina yake na Flora na familia yake ambao alisema umedumu kwa siku kadhaa.
     Mimi sijabaka na sijawahi kubaka; sijatenda dhambi yoyote; sijafanya kitu chochote na kibaya haya mambo yote ni ya kusingiziwa tu. Mungu wangu ni shahidi. Na kwa kuwa sijafanya hiyo dhambi kama wanavyodai, basi Mungu wangu atanitetea
    alisema Mbasha ambaye anaonekana zaidi kwenye video ya wimbo wa Maisha ya Ndoa alioshirikiana na mkewe Flora.
    Si wamesema wananitafuta, nitakwenda mwenyewe polisi. Nitawasikiliza na nitatoa maelezo yangu. Kama wakinipeleka mahakamani basi ukweli utajulikana... ipo siku kila kitu kitakuwa wazi.
    Kabla ya kufunguliwa kwa faili la tuhuma hizo, msichana huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala (Amana) ambako alifunguliwa faili la matibabu namba 667. Matokeo ya vipimo ambavyo vilifanywa na daktari kung'amua kama binti huyo aliingiliwa vinaonyesha kuwa kulikuwa na mbegu utokaji wa mbegu usio wa kawaida (HVD).
     Kadhalika binti huyo alifanyiwa vipimo kuona kama ameambukizwa virusi vya Ukimwi (VVU), pia kupata ujauzito, lakini matokeo ya awali yalionyesha kuwa yupo salama.


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.