June 02, 2014

  • MAJANGAZZ MUME AMPIGA MKE WAKE KWA MCHI KICHWANI KISA HAWARA




    MAJANGAZZ MUME AMPIGA MKE WAKE KWA MCHI KICHWANI KISA HAWARA
    Mke wa mtu anayefahamika kwa jina la Pamela Said (30) anayedai kupigwa mchi kichwani na mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la Alex.
     Mke wa mtu aliyejitambulisha kwa jina la Pamela Said (30) amedai kupigwa mchi kichwani na mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina moja la Alex kisa kikiwa ni simu aliyopigiwa mumewe na hawara'ke.Tukio hilo la kusikitisha lilijiri Mei 23, mwaka huu nyumbani kwa wanandoa hao, Mwembe-Supu, Ulongoni maeneo ya Gongo la Mboto, Dar muda mfupi baada ya kutoka kwenye bata ndefu usiku.
    Habari zilidai kwamba kabla ya kugeukia masumbwi, wanandoa hao walikuwa kwenye 'pub' yao iitwayo Milano iliyopo maeneo hayo wakijiachia kwa raha zao.
    Bi. Pamela Said akiwa katika maumivu makubwa.
    Kwa mujibu wa chanzo chetu, ilibainika kuwa siku hiyo majira ya saa 5:00 usiku, Alex, akiwa amepitiwa na usingizi simu yake iliita huku jina la Salima likionekana kwenye 'skriini'.
    Ilisemekana kwamba Salima aliwahi kuwa mfanyakazi katika pub yao ambapo Pamela alimtuhumu kuwa na uhusiano na mumewe.
    Bw. Alex, mume wa Pamela Said.
    Ilidaiwa kuwa Pamela alimuomba mumewe wakamtimua kazi Salima lakini amekuwa akiendeleza uhusiano huku akipiga simu mara kwa mara hasa usiku kitendo ambacho kilimchukiza Pamela. 
    Ilidaiwa kuwa baada ya kuona simu hiyo, Pamela alimuamsha mumewe ambaye alipokea simu hiyo na kuanza kujikanyaga na kukata simu ndipo alipompigia kwa namba yake na kuanza kujibizana huku akipokea maneno ya karaha bila kutegemea mazungumzo hayo yalimtia hasira Pamela ambaye alimuuliza kwa hasira mumewe huku akitaka kujua kuna nini kati yake na huyo Salima.Soma zaidi hapa>>>>>>>


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.