Liberatus believes "CHARITY STARTS AT HOME"
Katika muendelezo wa kusaidia nyumbani kama imani yangu ya kimsingi; ninaamini kuwa, "binadamu tulizaliwa tushirikiane na tusaidiane kutatua matatizo na sio kutengana wala kushindana."
Mgombea wa Uraisi wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwna Liberatus Mwago'mbe wakwanza (kusoto) akiwa na Dr. Kingslaw (wa katikati) na Nurse kabla ya lecture katika hospital ya muhimbili Kwenye safari yangu ya Tanzania 2011 na 2013 nilipata fursa ya kutembelea hospital za Muhimbili na Aga Khani zilizopo Dar Es Salaam, na hospital ya Muhimbira iliyopo kijijini kwetu Chimala, Mbeya. Kwenye hospital ya Muhimbili na Aga Khan niliongozana na Dr. Les Kingslaw (A Pulmonologist from Wshington Hospital and Providence Hospital) na Ms. Kingslaw (Nurse practitioner).
Safari ya Muhimbili na Aga Khan, year 2011
Dr. Kingslaw akiendelea kutoa somo la ugonjwa wa COPD Aga Khan
Katika safari hii Dr. Kingslaw alitoa somo juu ya ugonjwa wa Chronic Obstractive Pulmonary Disease (COPD) unao sababishwa na uvutaji wa sigara kwa asilimia kati ya 80-90%. Ugonjwa huu husababishwa pia na mambo mengine, kama vile, genes, historia ya familia, kazi unayofanya na mazingira; lakini husababishwa na utumiaji tumbaku (sigara) kwa asilimia kati ya 80-90%.
Baada ya kutoa somo juu ya gonjwa hili, COPD, tuliweza kutoa vipimo vya oxygen kama msaada. Vipimo hivyo vinaitwa "pulse oximetry". Vile vile nilipata kubadilishana mawazo na madaktari wa Muhimbili na Aga Khan. Mgombea wa Uraisi wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwna Liberatus Mwago'mbe akiwa na Mr. & Ms. Kingslaw na daktari wa Aga Khan baada ya lecture Katika mabadirishano ya mawazo; nilishtushwa na ukweli kuwa kuna watu hupoteza maisha kwa sababu tu, hawawezi kulipia mtungi wa oxygen! Baada ya mazungumzo hayo; nilirudi USA na kuendelea kupiga "box" huku nikitafakari jinsi ya kutatua matatizo haya.
Bado tafakuri hili linaendelea na naomba ushirikiano wa waTanzania wote waliopo USA kufanya jambo lolote kwaajili ya nyumbani.
Safari ya hospital ya Muhimbira Chimala Mbeya, year 2013
Mgombea wa Uraisi wa Jumuiya ya waTanzania DMV Bwna Liberatus Mwago'mbe anarudisha kidogo alicho nacho kwenye hospital ya kijijini kwao
Hii ni kati ya hospital masikini nilizo tembelea. Niliona mengi ambayo yanatakiwa kuwezeshwa. Hospital ya Muhimbila hutoa huduma kwa watu zaidi ya 20,000 kwa mwaka! Hospitali hii inaupungufu wa vifaa mbalimbali vya kutendea kazi; kama vile, vitanda, sindano, dawa za maleria, vipimo vya X-ray, oxygen tanks n. k. Hii ni hospital niliyo kuwa natibiwa maleria kipindi nikiwa mdogo.
Sikusita kupita na kutoa kidogo nilicho jaliwa. Nilipo enda nyumbani mwaka 2011 waliniambia kuwa wanaupungufu wa vifa vya kutendea kazi, kama vile kipimo cha "Blood Presssure". Mwaka 2013 nilipo kwenda niliwapelekea kipimo hicho cha mapigo ya moyo na chenye uwezo wa kupima "heart rate". Daktatri na wauguzi (nurses) walifurahi sana.
Naitwa Liberatus Mwang'ombe "Libe" kwa unyenyekevu wa dhati naomba tushirikiane na unipigie kura
Asante sana kwa kusoma makala yangu fupi ya kutembelea hospitali nyumbani Tanzania
Libe for The DMV Community President 2014
0 comments:
Post a Comment