June 16, 2014

  • MKUU WA WILAYA YA MAKETE ATOA RAI KWA JAMII YA MAKETE KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI


    MKUU WA WILAYA YA MAKETE ATOA RAI KWA JAMII YA MAKETE KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI
     Mkuu wa wilaya ya Makete mwenye suti nyeusi (aliyesuka nywele) Mh. Josephine Matiro, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (kulia kwa mkuu wa wilaya) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto walioshiriki maadhimisho hayo.
     Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro(wa tatu kushoto walioketi) na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (wa pili walioketi kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa shirika la wasaidizi wa kisheria Makete
     Katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Iwawa Makete ambao nao walishiriki
     Wanafunzi wa shule ya msingi Ndulamo wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha/habari na Edwin Moshi na Conrad Mpila, Makete.)
    Imeelezwa kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali peke yao kufanya kazi hiyo
     
    Kauli hiyo imetolewa leo hii Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika viwanja vya mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe.
    Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio wengi Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira magumu ambao wanahitaji msaada wa kila mmoja

    "Ni kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu, hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya uwezo wake, mwenye sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya hivyo kwa wakati wake" amesema Matiro

    Katika risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang'anya misaada wanayopewa na wadau mbalimbali

    Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu.
    Hivyo amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia.
    Katika maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa  na kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
     Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo" 


  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.