June 11, 2014

  • JOSE MOURINHO ATAMBA: TAYARI CHELSEA TUMEMNASA CESC FABREGAS



    JOSE MOURINHO ATAMBA: TAYARI CHELSEA TUMEMNASA CESC FABREGAS
    JOSE MOURINHO ATAMBA: TAYARI CHELSEA TUMEMNASA CESC            FABREGAS

    JOSE Mourinho anaamini kwamba tayari amemnasa Cesc Fabregas kutoka Barcelona kama mbadala wa Frank Lampard ndani ya Chelsea na anatumai dili litakamilika kabla Hispania haijaikabili Holland Ijumaa hii katika mchezo wao wa ufunguzi wa kombe la dunia.

    Kocha huyo wa Chelsea yuko na matumaini makubwa kuwa Fabregas na mshambuliaji wa Atletico Madrid, Diego Costa wanatua Stamford Brdige kiangazi hiki ikiwa ni juhudi zake za kuimarisha safu yake ya ushambuliaji kwaajili ya msimu ujao.

    Chelsea ilimaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita wa Ligi Kuu ya England, pointi nne nyuma ya mabingwa Manchester City ambapo muda wote Mourinho alikuwa akisema wao hawako kwenye ushindani wa kusaka taji.

    Inaaminika usajili wa Fabregas na Costa, unaotarajiwa kuwagharimu £28m na £32m, utaisaidia Chelsea kushinda taji lao la kwanza la Ligi Kuu tangu msimu wa 2009-10.



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.