ya Jamii, Tabora 
        MKUU wa Jeshi la Polisi                hapa nchini IGP Ernest Mangu ameteua timu ya askari polisi                wataochunguza tuhuma za wizi wa fedha za wakulima wa zao                la tumbaku katika vyama vya ushirika vya wakulima hao                mkoani Tabora. 
         IGP Mangu amemteua                Kamishna wa Polisi Issaya Mngulu (pichani) ambaye ni                Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai hapa nchini                kuongoza timu. 
         Timu hiyo ya upelelezi                kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam                tayari imewasili mkoani hapa kuanza kazi ya kuchunguza                ubadhirifu huo unaofanyika katika vyama vya msingi vya                wakulima wa tumbaku. 
         Akitoa taarifa kwa                waandishi wa habari mara baada ya kuwasili mkoani hapa                Kamishna Mngulu alisema timu imeundwa kutokana na agizo la                Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la tarehe 7/6/2014                alipokuwa ziarani mkoani hapa baada ya kuguswa na kilio                cha wizi mkubwa wa fedha za wakulima wa tumbaku. 
         Mngulu alisema timu                hiyo ni maalumu na imekuja mahsusi kwa ajili ya kuchunguza                wizi wanaofanyiwa wakulima wa tumbaku kupitia vyama vya                msingi mkoani hapa Alifafanua kuwa timu hiyo inaanza kazi                mara moja kwa kuchunguza chama kimoja hadi kingine ili                kubaini wizi na hujuma zote zilizofanyika na zinazoendelea                kufanyika ambazo zimekuwa kero kwa wakulima wa zao hilo                katika mkoa wa Tabora. 
         'Natoa rai kwa wananchi                wa mkoa wa Tabora kutoa ushirikiano kwa timu hii mara                watakapohitahika ili kuwezesha mafanikio ya kazi hii kwa                wakati mwafaka, kazi hii ni ngumu lakini tutaifanikisha                kwa ushirikiano wa wananchi na wadu wengine, aliongeza.
        
 
 
.jpg) 
 
 
0 comments:
Post a Comment