Wito                  umetolewa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan                  wazazi wenye watoto  walio na umri chini ya miaka 5                  kuhakikisha kuwa  wanashiriki kikamilifu katika zoezi la                  utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za Minyoo kwa                  kuwapeleka watoto wao katika vituo mbalimbali vya afya                  ili waweze kupatiwa dawa hizo kabla ya terehe 20 mwezi                  huu.
           Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck                  Sadiki ametoa wito huo leo jijini Dar es salaam kufuatia                  zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A na dawa za                  minyoo  kwa vituo vyote vya kutolea huduma vya Serikali,                  binafsi na mashirika ya dini  vilivyoainishwa katika                   manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni kuelekea mwisho.
          Amesema                   zoezi hilo lililoanza tarehe 7 mwezi huu  ni sehemu ya                  utekelezaji wa mkakati  wa Lishe wa Taifa  uliozinduliwa                  na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2013  kwa lengo la kuongeza                  kasi ya uwajibikaji katika kuongeza hali ya lishe                  nchini.
          "Zoezi                  hili sio geni kwani ni utaratibu ambao sote tunaufahamu                  kuwa Serikali yetu kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa                  Jamii kwa kushirikiana na wadau wa Afya huendesha zoezi                  huendesha zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A na                  dawa za Minyoo kwa watoto walio na umri chini ya miaka 5                  nchi nzima  kila mwaka"
          Amesema                  zoezi la utoaji wa dawa hizo ni muhimu kutokana na                   miili ya watoto hao kuwa katika mahitaji makubwa ya                  vitamin A kutokana na mchango wake  katika ukuaji wa                  miili na akili kwa kuimarisha uwezo wa kinga zao dhidi                  ya magonjwa pamoja na kuimarisha uwezo wa macho.
          Kwa                  upande wake mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt.                  Grace Magembe akizungumza kuhusu zoezi hilo ambalo                  linafikia kilele chake tarehe 20 mwezi huu amesema kuwa                  ni vema jamii ikawa na mwitikio chanya kwa zoezi hili                  kutokana na umuhimu wake  kwa watoto walio na umri chini                  ya miaka 5.
          Amesema                  kuwa zoezi la utoaji wa matone ya Vitamini A huokoa                  maisha ya watoto kwani huwalinda na dhidi ya maradhi                  hatari kama vile Kuharisha, Surua na maradhi ya mfumo wa                  hewa.
          "Kila                  mzazi anatamani kumuona mtoto wake anakua akiwa na afya                  njema, watoto wenye upungufu wa Vitamini A wapo katika                  hatari ya kuugua maradhi,kupata upofu na hata kupoteza                  maisha" Amesisitiza.
          Aidha,                  amesisitiza kuwa dawa zinazotolewa katika zoezi hilo ni                  salama kwani tayari zimepitishwa na Wizara ya Afya na                  Ustawi wa Jamii na kuthibitishwa na Mamlaka ya Chakula                  na Dawa nchini (TFDA) na Shirika la Afya Duniani (WHO).
          "Nawasihi                  wananchi mjitokeze kwa wingi katika zoezi hili kwa siku                  zilizobaki kwa kuwa zoezi hili tunaloliendesha ni                  salama"
         
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment