June 02, 2014

  • JESHI LA MAGEREZA KUINGIA USHIRIKIANO RASMI NA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

    Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara alipowasilishwa katika ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (kulia).
    Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete (wa tatu) wakisani hati za makubariano ya ushirikiano kati ya Taasisi hizo mbili. Wakwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa na wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango anayeshughulikia Teknolojia na Huduma za Kujifunzia Chuoni hapo.
    Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt Juma Malewa(wa kwanza kulia) na Prof. Modest Valisango (wa kwanza kushoto) wakisaini hati za makubaliano ya ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
    Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja ( kulia) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Prof. Tolly Mbwete ( kushoto)wakibadilishana nyaraka muhimu za makubaliano ya ushirikiano mara baada ya kutiwa sahini.
    Kamishna Jenerali wa Magereza John Minja (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo.
    Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria (wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya undani wa ushirikiano kati ya Jeshi la Magereza na Chuo Kikuu Huria.Wa kwanza kulia ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza nchini Dkt. Juma Malewa, wa nne kulia ni Naibu wa Tatu wa Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Modest Valisango aliyepia Mkuu wa Teknolojia na Huduma za Mafunzo chuoni hapo. 

    Aliyewahi kuwa mfungwa kwa takribani mika 20 gerezani Ukonga Ng. Haruna Pembe (mwenye suti) akitoa ushuhuda wa jinsi alivyoweza kusoma na kumaliza shahada yake ya sharia akiwa gerezani.Picha zote na Insp Deodatus Kazinja, PHQ
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.