May 12, 2014

  • MASTAA WA BONGO KUMSHITAKI MPOKI

     

    KIMENUKA! Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa mwanasheria wao, Ijumaa Wikienda lina ishu nzima.

    Mujuni Silvery 'Mpoki'.
    Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club inayomiliki Bendi ya The African Stars 'Twanga Pepeta', Asha Baraka, mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'.
    Aisha Mashauzi.
    Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Aisha Ramadhani 'Mashauzi', Maria Sarungi na DJ Bonny Love.
    WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
    Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata nafasi ya kujitetea (balansi).
    Asha Baraka.
    "Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama mnavyofanya magazetini.
    "Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si mwingine," kilisema chanzo hicho.
    Maimartha wa Jesse.
    MADAI YAO YA MSINGI
    Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao  kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki.
    KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
    Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka.
    MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
    ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano.
    RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans.
    Wema.
    KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
    WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi!
    VANESSA; alimwambia afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si vyema kuyaandika hapa).
    WIKIENDA LAWASAKA   
    Baada ya madai hayo, gazeti hili liliwasaka mastaa hao mmojammoja ili kusikia ukweli wa madai hayo.
    Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka Kadinda juzi ambapo simu yake haikuwa ikipatikana hewani kama alivyozoeleka.
    Kwa upande wake Ray alikiri kuwepo kwa uwezekano wa kumshitaki kwa kuwa ni kweli alimdhalilisha mbele ya kadamnasi.
    Naye Mai alipotafutwa aliwaka akidai kuwa alichokifanya Mpoki hakikuwa sahihi kisheria hivyo jambo hilo lipo.
    Ray Kigosi.
    Kwa upande wake, Isha Mashauzi alisema kuwa labda wenzake wameamua kumshtaki Mpoki lakini hawakuwa wamemjulisha. Mastaa wengine ambao simu zao ziliita bila kupokelewa ni Asha Baraka, Vanessa, Wema na DJ Bonny Love.
    MSIKIE MPOKI
    Mpoki alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu malalamiko ya mastaa hao, katika hali ya kushangaza alisema hakumbuki nini kilitokea siku hiyo.
    "Kusema ule ukweli mimi sikumbuki chochote kile kilichotokea siku ile, we  nitajie majina ya hao watu niwapigie halafu baadaye ndiyo tutaongea," alisema Mpoki akiweka sharti hilo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwananga jukwaani.
    Martin Kadinda.
    ATUMA MESEJI YA HASARA!
    Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mpoki baada ya kupigiwa simu saa saba alasiri na kujibu hivyo, usiku wa saa mbili alituma meseji kwa mwandishi iliyosomeka:
    "Hapo ndipo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia? Sijui lini mtafika kikomo cha kuwa watumwa wa ujinga… Nisichokijua hakiwezi kunisumbua..."
    AKIKUTWA NA HATIA KISHERIA
    Kwa mujibu wa mwanasheria mmoja (jina tunalo) aliyezungumza nasi, endapo Mpoki akipanda mahakamani na kukutwa na hatia, anaweza kufungwa kifungo cha miaka 5 jela au faini kulingana na uzito wa udhalilishaji huo kwa mujibu wa walalamikaji.
    GPL
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.