June 21, 2014

  • UINGEREZA YAFUNGASHIWA VIRAGO, ITALY TIA MAJI TIA MAJI KWA KUPIGWA 1-0 NA COSTA RICA



    UINGEREZA YAFUNGASHIWA VIRAGO, ITALY TIA MAJI TIA MAJI KWA KUPIGWA 1-0 NA COSTA RICA
     Na Sultani Kipingo
    Wakiwa wameshinda mara mbili katika michezo yao ya kwanza ya Kombe la Dunia 2014, Costa Rica wamedaka tiketi ya kwenda katika raundi ya mtoano ya 16 huku Brazil.
     Baada ya kufanya maajabu kwa kuifunga Uruguay katika mchezo wao wa fungua dimba, Costa Rica wamaeitungua Italy 1-0 leo katika mchezo mkali wa kundi D katima uwanja wa Pernambuco mjini Recife.
     Goli lao la ushindi limepatikana dakika chache kabla ya mapumziko pale kiungo wao mahiri Bryan Ruiz alipotia ndinga kimiani kwa kichwa kufuatia majalo tamu ya kona ya Junior Diaz.
    Mpira huo baada ya kupigwa kichwa na Ruiz uligonga besela na kudunda ndani ya goli. Teknolojia mpya ya kugundua magoli ilithibitisha hilo ni bao kwani mpira ulishavuka mstari. Matokeo hayo yanaihakikishia Costa Rica nafasi katika raundi ya 16 bora na hapo hapo wanakuwa wameifungashia virago Uingereza.Ushindi huo pia umeongeza kasi ya ushindani baina ya Uruguay na Italy watapokutana Juni 24, ambapo wote walishamchapa Uingereza, na wote wamechabangwa na Costa Rica, na ushindi wowote baina yao utampleka aliyeshinda hatua inayofuata. Ila Italy ndiyo yenye matumaini zaidi kwani ina magoli zaidi.... 



  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.