Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa Uganda, Balozi James Mugume,
amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo ilivyowekewa na Marekani kama
hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.Kwa mujibu wa BBC,
Balozi Mugume ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya
mazungumzo na Marekani ili kufafanua hatua waliyochukua.Amesisitiza
kuwa wataieleza Marekani sheria hiyo inapinga tabiaambayo sio ya
kiafrika na maadili ambayo hayakubaliki katika jamii nyingi za
kiafrika.Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo havitakuwa na athari
kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika ya kijamii
kuwatayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya wapenzi
wa jinsia moja
0 comments:
Post a Comment