Kuna Utapeli umeanza        kusambaa saa chache zilizopita kupitia CRDB INTERNET BANKING .
      Anayefanya utapeli huu        ametengeneza majina bandia ya watu maarufu kama wanasiasa na        wanamuziki kisha anaingiza watu kwenye contact list yake halafu        anawatumia ujumbe huu kama vile yeye ni mtu halisi .
      Mtu anapokubali anampa huyu        jamaa taarifa zake za benki halafu mwisho wa siku hela zake        zinaweza kuhamishwa kwa njia ya mtandao .
      MFANO WA UJUMBE NI HUU
      ----------------------------------------------------- 
      Habari za wakati ndugu        watanzania! Kwa yoyote ambae amejiunga na huduma ya CRDB Bank        kupitia Online. Internet Banking sio SIM BANKING alie jiunga na        Internet Banking. Tafadhali naomba tuwasiliane kuna project maalum        yenye faida kwangu nakwako pia kwa kushirikiana nao CRDB Bank.        Malipo ni kila wiki katika hiyo project. Nitumie meseji inbox kama        umejiunga na internet banking na unahitaji kushiriki katika hii        project
      ==============================================================  
      Mpaka sasa hivi nimegundua        majina 2 ya Kala Jeremia ambaye ni mwanamuziki na Jerry Silaa        ambaye ni mwanasiasa .
      Tuchukuwe tahadhari na        tusambaze ujumbe huu .
    
0 comments:
Post a Comment