FT: TAIFA STARS 1 : 0 ZIMBABWE
Dakika 90` zimeshamalizika Taifa stars wameshinda bao 1-0.
Dakika za lala salama Zimbabwe wanashambulia kwa kasi.
Dakika 45` za kipindi cha pili zimeshakatika na mwamuzi anaongeza dakika 4.
Dakika ya 43` kipindi cha pili Taifa stars bado wanaongoza kwa bao 1-0.
Dakika lala salama mpira ni wa kasi mno hapa uwanja wa Taifa, Zimbabwe wanahitaji kusawazisha.
Dakika ya 40` Hamis Mcha `Vialli` anaingia kuchukua nafasi ya John Bocco.
Dakika ya 39` Taifa stars wanaongoza na Zimbabwe wanachezza kwa haraka haraka.
Dakika ya 37` kipindi cha pili, heheeeeh! hatari sana, Zimbabwe wameikosa Stars hapa.
Dakika ya 36` kipindi cha pili, Mbwana aliingiza pasi nzuri ndani ya eneo la hatari la Zimbabwe, lakini hakuna wa kumalizia.
Zimbabwe sasa wamerudi mchezoni na wanacheza kwa kufungaka tofauti na kipindi cha kwanza walipojibana eneo lao. Mzani wa mpira unakwenda sawasawa.
Kona inapigwa na Zimbabwe , mabeki wa stars wanaokoa.
Mrisho Ngassa anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Harun Chanongo.
Dakika ya 30` kipindi cha pili Zimbabwe wanapiga kona, lakini kipa Dida anacheza vizuri na kuwa kona nyingine.
Dakika ya 29` kipindi cha pili Zimbabwe wanapata kona lakini Stars wanaokoa.
Dakika ya 28` kipindi cha pili Taifa stars bado wanaongoza kwa bao 1-0.
Frank Domayo anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Amri Kiemba. Ilitegemewa Mwinyi angekwenda benchi lakini imekuwa tofauti. Mwalimu Nooij anajua kwanini amefanya hivyo.
Dakika ya 23` kipindi cha pili, Taifa stars wanaongoza kwa bao 1-0.
Mpira umesimama, kocha wa Stars Mart Nooij anazungumza na wachezaji wake, yupo Mwana Samata na wengine.
Nidir Haroub anaonesha uzoefu wake kwa kuosha kila mpira unaokuja. Anatumia staili ya beki hasifiwi chenga.
Dakika ya 19` kipindi Stars wanashambulia, lakini inakuwa goli kiki.
Dakika ya 17` kipindi cha Mwinyi Kazimoto yuko chini anagangwagangwa .
Dakika ya 16` kipindi cha pili kiungo Amri Ramadhani Kiemba ananyanyuliwa na anapasha moto misuli.
Kwa dakika hizi, Sehemu ya kiungo ya Taifa stars kuna haja ya kocha Mart Nooij kufanya madiliko kwasababu wamepwaya. Nadir Haroub `Canavaro` anajitolea sana.
Dakika ya 13` kipindi cha pili, Stars wanaongoza kwa bao 1-0.
Dakika hizi 11` za kipindi cha pili Zimbabwe wanacheza kwa nafasi na kama Stars hawatabadilika kiuchezaji basi itakuwa hatari sana.
Dakika ya 10` kipindi cha pili Zimbabwe wanakosa bao baada ya Dida kusimama vizuri.
Dakika ya 9` kipindi cha kwanza bado Stars wanaongoza.
Dakika ya 7` kipindi cha pili, Mbwana Samata aliachia shuti kali mno, lakini kipa wa Zimbabwe ameokoa.
Dakika ya 4` kipindi cha pili John Bocco anakosa nafasi nyingine ya kufunga goli.
Dakika ya 2` kipindi cha pili, John Bocco anakosa bao la wazi baada ya kushindwa kumalizia krosi ya chinichini.
Dakika ya kwanza tu Taifa stars wamekosa bao na Zimbabwe wamekosa bao vilevile.
Kipindi cha pili kimeanza hapa uwanja wa Taifa
HT: TAIFA STARS 1 : 0 ZIMBABWE- Bao la stars lilifungwa na John Bocco.
Dakika 45` zimeshamalizika na mwamuzi ameongeza dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 40` kipindi cha kwanza Taifa stars bado wanaongoza kwa bao moja.
Kwa dakika 3` mfululizo, lango la Taifa stars limekuwa katika hatihati kubwa.
Dakika ya 31` kipindi cha kwanza Zimbabwe almanusura waandike bao baada ya kipa Deo Munish kujigonga mwenyewe.
Dakika ya 28` kipindi cha kwanza Mwinyi Kazimoto anajaribu kupiga shuti kali, lakini kipa anaokoa na mpira ni kona haizai matunda.
Dakika ya 22` kipindi cha kwanza Taifa stars wanaongoza kwa bao moja lililofungwa na mshambuliaji John Raphael Bocco `Adebayor`.
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
TAIFA STARS 1 : 0 ZIMBABWE
0 comments:
Post a Comment