May 19, 2014

  • BALAA JINGINE GEITA!! KIJANA AJINYONGA HADI KUFA KWENYE CHOO CHA MAMA MKWE WAKE,ALITAKA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE AKAKIMBIWA NA MKEWE

     
     
     

    Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Daudi James(33) mkazi wa mtaa wa Shilabela mjini Geita mkoani Geita amekutwa amekufa kwa kujinyonga chooni kwa mama mkwe wake kwa kutumia kitenge.

    Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea usiku wa kuamkia leo ambapo Daud James amekutwa amejinyonga chooni kwa mama mkwe wake eneo la General Tyre.

    Akizungumzia tukio hilo mama mkwe wa marehemu Lucia Magulu(32) amesema marehemu alimuoa binti yake Dorothea Jacksoni(18) mwaka mmoja uliopita huku akiwa na ujauzito wa mwanamme mwingine na baada ya kujifungua wameendelea kuishi na mtoto wao ambaye ni Hellena mwenye umri wa miezi kumi.

    Akiendelea kusimulia mkasa huo amesema binti yake Dorothea Jacksoni(18) walikuwa wamehitlafiana na mme wake na kurudi nyumbani takribani zaidi ya mwezi mmoja kwa sababu za marehemu mme wake kuwa anamutaka mkewe wafanye tendo la ndoa kinyume na maumbile ndicho kilichomfanya arudi nyumbani.

    "Jana jioni alipofika hapa nyumbani alikaa hadi walipomaliza kula chakula cha jioni na alipoambiwa arudi nyumbani kwake Shilabela alikataa na kutaka aende na mke wake ",anaeleza mama mkwe.


    "Baadae mke wake alipomkatalia kwenda marehemu alimuomba kitenge mke wake kwa maelezo ya kuwa anaenda kulala kwa rafiki zake na ndipo alipopewa,cha kushangaza na kusikitisha leo asubuhi tumemkuta kajinyonga kwa kitenge hicho chooni",ameongeza mama mkwe.


    Kamanda wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa

    uchunguzi bado unaendelea ili kubaini sababu gani zilipelekea kifo chake.


    Hata hivyo kamanda Konyo ameitaka jamii kuacha mambo ya kujichukulia maamuzi ya kujiua bila sababu za msingi huku akiwataka waandishi wa habari nao kuelimisha jamii iachane na tabia za kujinyonga kila mara wanapokuwa wamezozana na wake zao.


    Hili ni tukio la pili kutokea ndani ya siku tatu ambapo juzi mkazi wa tambukareli mjini Geita alijinyonga na kijining'iniza kwenye mti wa mpera baada ya kuhitlafiana na mke wake.
  • 0 comments:

    Post a Comment

    Copyright @ 2013 Michapo | Kisiwa cha Habari.